Akizungumza na eNewz ya EATV, Msami ameonesha kukerwa na kauli ya AT iliyodai kuwa wanaobebwa kwenye muziki ni wale wanao 'dance' huku wakiwa hawajui kuimba.
Katika hatua nyingine msanii huyo ameongeza kwamba AT hana ubora wowote kikazi ndiyo maana hawezi kuleta changamoto na wala hajawai kufikiria kufanya naye kazi, huku akimkumbusha kuwa hao anaowaita wacheza show huwa anawatafuta kipindi anapokuwa anawahitaji kikazi.
"AT anaongea tu kawa sababu hao dancers anaowasema yeye wana maisha nazuri kuliko yeye, wana fanbase kubwa na wanafanya maendeleo kibao kwa kutumia vipaji vyao. Lakini cha ajabu sisi ambao ni madancers watu wanapenda muziki wetu na tukipanda stejini watu wana enjoy, kwa kuwa unawaimbia na bado unawaburudisha . Lakini hapo hapo bado alikuwa ananipigiaga simu nimtafutie wacheza show akiwa na kazi" . alisema Msami.

Msami
Aidha Msami ameongeza kwa kuwataja wasanii kutoka kundi la Makomando kwamba ni wabunifu lakini wakati huo huo wana uwezo mkubwa wa kuimba kuliko AT hivyo inampasa kuwaheshimu hao anawaita ma -'dancers' kwa sababu Mungu pekee ndiye ameamua wafike walipofikia.
Msamii anayetamba na ngoma mpya ya 'So Fine' amesema yeye kabla ya kuanza kuimba alikuwa mcheza show na mafanikio makubwa aliyapata kupitia kazi hiyo kama kununua gari lake la kwanza, kujenga nyumba na kuhudumia familia yake hivyo kumtaka AT asizungumze mambo asiyoyajua.
