Saturday , 1st Nov , 2014

Msanii wa muziki Amin Mwinyimkuu, ambaye amepitia wakati mgumu kwa kuondokewa na ndugu zake katika kipindi cha miezi mitatu mfululizo, ameweka wazi kuwa jambo hili limemfanya kuwa mtulivu kutafakari maisha.

Amini

Amin abaye wiki hii ameadhimisha siku yake ya kuzaliwa bila party yoyote kutokana na majanga haya, amesema kuwa amelazimika kutulia kutafakari, japokuwa anaendelea kufanya muziki ambao ndio unamuweka mjini.

Staa huyu amewataka mashabiki wake kufahamu pia kuwa, ndani ya wiki chache kutoka sasa, atawapatia mashabiki wake zawadi ya ngoma mpya.