Monday , 16th Nov , 2015

Producer Mazuu kutoka Mazuu records amesema mfumo wa muziki uliopo nchini unafanya wasanii wachanga wasitoke kimuziki, na kubaki kushikiliwa na wasanii maarufu.

Mazuu ameyasema hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio na kueleza kuwa iwapo msanii mchanga mwenye kipaji hana pesa za kutosha kujitangaza, hataweza kufanikiwa kutokana na mfumo kuwajali wale wenye pesa.

"Leo hii muziki watu wengi wanaangalia wale walio tayari masuper star, hawaongelei msanii ambaye anakuja, mchanga, kwa sababu huwezi kuwa super star bila kuanza chini, Je? huyu ambaye anatoka chini amejengewa misingi gani?", alisema Mazuu.

Mazuu aliendelea kusema kwamba iwapo wasanii wachanga wangepata msaada wa kutosha, ingekuwa rahisi kwa wao kutambulika na kupata msaada mkubwa zaidi na hatimaye kuwa wasanii wakubwa.

"Leo hii kwa kuwa ushaambiwa sanaa ina hela, ukiangalia msanii mchanga anataka kutoka kweli ana nyimbo nzuri hana budget ya kutosha ya kuweza kufanya promotion, hana management hana kila kitu, lakini huenda angepatiwa nafasi ya ngoma yake kulia, wangejitokeza watu kama management, angepata watu wa matangazo, of course nae angeweza kumanage hata kile kipaji chake na akweza kufika mbali", alisema Mazuu.