
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo mchungaji Mashimo amesema kwamba alifanya hivyo kwa kuwa alitumwa, na aliyemtuma ni Mungu.
“Kweli nimehusika kuwatoa, hata magereza ni mimi nilienda, jambo la msingi mjue kwamba Amber Ruty ni mtoto wa Mungu, nisipotumika siwezi kuwa mtumishi wa Mungu, ila ni kweli natumiwa, natumwa na Mungu”, amesema Mchungaji Daudi Mashimo.
Hata hivyo Mchungaji Mashimo amesema ana mengi ya kuyaongea kuhusu Amber Ruty, mpenzi wake na msanii Wema Sepetu, lakini wakati muafaka utakapofika ndipo atazungumza ili watanzania waweze kufahamu