Thursday , 27th Mar , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Fille pamoja na meneja wake MC Kats wameibuka na jipya baada ya msanii huyu kutangaza kuwa hayupo tena chini ya usimamizi Kats, taarifa ambazo Meneja huyu amezikanusha vikali.

Fille hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa Facebook aliwafahamisha mashabiki wake kuwa MC Kats sio Meneja wake tena, na wakati hili likifahamika hivi, MC Kats naye akaibuka na kudai kuwa yeye bado ni Meneja wa mwanadada huyu licha ya maneno watu wanayoongea, na kuwa kwa sasa wapo katika mpango wa kuachia ngoma mpya ambazo zinakwenda kwa jina Ur So Nice and Beta Tig with Aganaga.

Kufuatia taarifa hizi zinazopingana, bado haijafahamika hasa ukweli ni upi katika suala hili huku wengi wakiongeza kuwa, chanzo kinaweza kuwa ugomvi wa mapenzi ambao unaingiliana na masuala ya kazi zao.