Friday , 7th Nov , 2014

Jamila Vera Swai, mbunifu mahiri wa mitindo ya mavazi hapa Tanzania, amesema kuwa, kutengeneza mitindo ya mavazi hapa hapa Tanzania kwa kutumia wabunifu wetu wenyewe, ni hatua tosha ya kuonyesha na kuwakilisha utamaduni na asili yetu kupitia mitindo.

mbunifu wa mavazi nchini Tanzania Jamila Vera Swai

Mbunifu huyu ambaye naye pia atashiriki katika maonesho ya Swahili Fashion Week kwa mwaka huu, amesema kuwa katika kuthibitisha hili mitindo yake kwa mwaka huu itatangaza zaidi utanzania ikiwa ni mitindo rahisi na yenye kuendana na uhalisia.