Akizungumza kwa njia ya simu na East Africa Radio, Mbasha amesema mahakama imefikia hatua hiyo baada ya kugundua hana kosa lolote, na anamshukuru Mungu kwa Ushindi wake huo.
“kwa kweli Mungu ni mkubwaamesikia kilio changu, na hatimae leo nimeachiwa huru, nimepitia kipindi kigumu sana kwa kweli, nawashukuru sana kwa kuniombea, kunifariji na kwa kunisapoti kwa kipindi chote nilichokuwa na matatizo”, alisema Mbasha.
Emanuel Mbasha alikumbwa na tuhuma hizo mnamo mwezi Julai mwaka 2014, na kesi yake kuendeshwa katika mahakama ya Wilaya Ilala ambapo leo ndio imetoa hukumu ya kesi hiyo.




