Wednesday , 16th Dec , 2015

Msanii wa muziki mwenye umri wa kutosha katika gemu ya muziki Noorah, amesema kuwa mazingira yamekuwa yakimbana kuendeleza safari yake ya muziki, akihofia kushusha heshima yake kwa kukosea kufanya video.

Staa wa muziki nchini Noorah

Mkali huyo ameyasema haya huku akiwa anafahamu kuwa kwa sasa soko linahitaji video ambazo zimekuwa na gharama za juu.

Noorah, ametoa mfano wa rekodi zake kama 'Nikupe Nini', 'Acha Ushamba' na 'Chembavament' ambazo anaamini kuwa ziliharibika ukubwa wake kutokana na kukosa video, akiwa sasa anatafuta wawekezaji katika muziki wake ili kurejea katika nafasi yake.