Wednesday , 12th Aug , 2015

Nyota wa muziki Mayunga, ameeleza kuwa mkataba wake mnono wa kufanya kazi chini ya usimamizi wa Akon, bado haujaanza kutokana na nafasi ya staa huyo wa kimataifa kubana, hususan kupitia projekti yake kubwa ya kusambaza umeme Afrika.

nyota wa muziki nchini Tanzania Mayunga akiwa stejini na staa wa muziki Akon

Mayunga amesema kuwa, Mpango huo utaanza baada ya Akon kupata nafasi nzuri na yeye, akiwa sasa ameanza kutikisa chati ndani na nje ya nchi kupitia video yake kali ya wimbo wa 'Nice Couples' ambayo ilianza kupigwa nje ya nchi, kwa maneno yake akieleza kuwa haya ni matunda ya usimamizi mzuri.

Kuhusiana na yote hayo, Mayunga anaeleza mwenyewe akianzia na tathmini ya mapokezi ya rekodi yake hiyo.