Wednesday , 9th Apr , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Maurice Kirya baada ya kufanikiwa kuiweka vizuri biashara yake ya mgahawa huko nchini Uganda, ameamua kuongezea vionjo kwa kuwa anatoa burudani ya muziki wa Live mara moja kila mwezi ndani ya mgahawa huu.

Maurice Kirya

Maurice amesema kuwa, katika mpango huu ameweka utaratibu wa kua anaalika pia msanii mgeni ambaye naye atakuwa akitoa burudani ili kuwapatia mashabiki ama wateja, ladha tofauti ya burudani ya muziki wa Live.

Kirya ambaye ana utaalam mkubwa wa kulicharaza gitaa, amesema kuwa atakua akimwaga burudani ya aina hii katika mgahawa wake, mara moja katika kila alhamisi ya mwanzo wa mwezi, ikiwa kama zoezi endelevu.