Monday , 19th Oct , 2015

Nyota wa muziki wa nchini Uganda, Maurice Kirya amesema licha ya msaada wa hapa na pale kipesa ambao Rais Yoweri Museveni amekuwa akisaidia wasanii, anapaswa kukazia mambo muhimu zaidi ikiwepo utekelezaji wa sheria ya hakimiliki ya kazi za wasanii.

msanii wa muziki wa nchini Uganda Maurice Kirya

Kirya ambaye hakushiriki katika hafla ya wasanii iliyoandaliwa na Rais nchini humo mwishoni mwa wiki, amesema kuwa nia yake si kumshambulia Rais wala wasanii walioshiriki hafla hiyo, akionesha wazi wazi msimamo wake kuwa, tukio hilo linafunika picha halisi ya hali ya wasanii, akiweka wazi kuwa alikataa mualiko kujikita katika mambo muhimu kwa sanaa siku za mbeleni.

Rais Yoweri Museveni mwishoni mwa wiki alipata nafasi ya kukutana na wasanii wa nchi yake ambapo kati ya shughuli nyingine alitoa mchango wa shilingi milioni 400 za Uganda katika mfuko wa kuendeleza wasanii.