
Filamu hiyo ambayo ni mtitiriko wa vipindi kadhaa, imewashtua raia wa Marekani wakiwemo wasanii wenzake, ambao walionesha kutofurahishwa nayo, na kutoa maoni yao ambayo huenda yakamuweka pabaya msanii huyo mwenye sauti ya kipekee duniani.
Miongoni mwa wasanii ambao wamezungumzia hilo ni John Legend ambaye alikubali pia kuonekana kwenye filamu, amesema anawaamini wanawawake hao na kwamba R. Kelly amewaumiza watu wengi kwenye maisha yao.
To everyone telling me how courageous I am for appearing in the doc, it didn't feel risky at all. I believe these women and don't give a fuck about protecting a serial child rapist. Easy decision.
— John Legend (@johnlegend) January 4, 2019
Neyo naye alifunguka ya moyoni na kuandika kwamba kitendo cha R. Kelly kufanya vitendo hivyo ni vitu ambavyo haviwezi kukubalika, kwani ni muhimu kuwalinda watoto zaidi kuliko kuulinda muziki.
Rapper Meek Mill naye amesema baada ya kuangalia filamu hiyo ametokea kuchukizwa na R. Kelly, kwani anaamini kila kilichozungumzwa.
I’m not feeling R after watching that .... it’s so much filthy shit going on in this industry nobody will ever really speak on the wild shit because most of them could have docs like this or even worst done about them! https://t.co/4tJxRHvLbQ
— Meek Mill (@MeekMill) January 5, 2019
UTATA WAIBUKA JUU YA TUHUMA
Baada ya back vocal singer wa R. Kelly, Jovante Cunningham kusema kuwa R. Kelly alishawahi kufumaniwa akifanya ngono na marehemu Aaliyah kwenye basi la tour, mama mzazi wa Aaliyah BI. Diane Haughton alikanusha taarifa hiyo na kusema kwamba wao kama wazazi walikuwa bega kwa bega na mtoto wao kwenye ziara zake zote, na haijawahi tokea tukio hilo.
Ikumbukwe kwamba R. Kelly na Aaliyah walidaiwa kuoana kwa siri wakati Aaliya akiwa na miaka 15, hivyo walifoji vyeti aonekane ana miaka 18, jambo ambalo wenyewe walilikanusha kila walipohojiwa, na ndio ikawa chanzo cha marehemu Aaliyah kutopenda kuweka maisha yake binafsi kwenye mitandao.
Licha ya hayo, wasanii wakubwa kama Jay Z na Lady Gaga, wamekataa kuonekana kwenye filamu hiyo, ambayo inaaminika na wengi kuwa imetengenezwa ili kummaliza R.Kelly kimuziki.
Ikumbukwe kwamba miaka ya 2002 hadi 2007, R. Kelly aliwahi kutuhumiwa kuwadhalilisha kingono baadhi ya wanawake hadi kupandishwa kizimbani, baada ya kuonekana kwa video akimkojolea mwanamke, na mwingine kudai kuwa alimuambukiza ugonjwa wa zinaa, na mashtaka mbali mbali ya kujihusisha kingono na wasichana ambao wako chini ya umri, kesi zote hazikumtia hatiani na kumuacha huru.
Baada ya kuachwa huru kutokana na tuhuma hizo, R. Kelly aliandika nyimbo mbali kali zilizofanya poa zaidi, ikiwemo alum ya Happy People na Yoo Saved me, ambayo wengi waliamini ni shukrani yake baada ya kunusurika kufungwa.
Hata hivyo baadhi ya watu nchini Marekani wameonesha kusikitishwa na kuchukizwa na malalamiko juu ya R. Kelly, wakiamini kwamba malalamiko yao hayatiliwi maanani kutokana na ubaguzi wa rangi, kwani katika matukio yote anayolalamikiwa kuyafanya, hakuna lililotolewa na binti mweupe.