Wednesday , 8th Jul , 2015

Staa wa muziki wa nchini Uganda Eddy Kenzo ambaye ametua nchini humo akitokea Marekani baada ya kujishindia tuzo kutoka BET apongeza mashabiki waliompokea na alishindwa kujizuia akitokwa na machozi kutokana na mapokezi hayo makubwa.

msanii nyota wa Uganda Eddy Kenzo akitokwa na machozi baada ya kupokelewa na mashabiki uwanja wa ndege

Eddy ameelezea kuwa kwa miaka mingi alikuwa akiona mashindano hayo ya tuzo za BET kupitia kwenye Televisheni pekee na hakudhania kuwa ipo siku Mungu angemfungulia milango kuweza kutimiza ndoto zake kuchaguliwa kutwaa tuzo za BET nchini Marekani.

Mchumba na mama mtoto wake Rema Namakula alikuwapo na baadhi ya marafiki, ndugu waliojikusanya katika uwanja wa ndege kumlaki nyota huyo anayetesa na kibao chake cha 'Sitya Loss'.