Man Water
Baada ya mtayarishaji muziki Sheddy Clever kulalamika kukosa tuzo ya mtayarishaji bora wa muziki wa kizazi kipya huku kazi aliyotengeneza ikichukua tuzo ya wimbo bora wa kizazi kipya wa mwaka, na kutoa kauli kuwa hata Man Water ambaye ndiyo ameshinda tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Muziki wa kizazi kipya kwa mwaka huu anafahamu kuwa hakuwa ana stahili tuzo hii, Man Water mwenyewe ameamua kufunguka juu ya maneno ya Sheddy Clever.
Mtayarishaji muziki huyu kutoka Combinations Sound amesema kuwa, kushinda kwake tuzo hii licha ya kuchangiwa na mashabiki pia kunatokana na kazi zake kufanya vizuri, na hapa anaeleza zaidi juu ya kauli aliyoitoa Sheddy Clever dhidi yake.