Tuesday , 29th Sep , 2015

Msanii Hisia amesema majukumu ya kazi zake ndizo yanayo sababisha yeye kutopanda kwenye jukwaa lolote la kisiasa kama ilivyo kwa wasanii wengine, na kumsapoti mgombea Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo Bi. Anna Mghirwa, ambaye ni mama yake mzazi.

Msanii Hisia amesema majukumu ya kazi zake ndizo yanayo sababisha yeye kutopanda kwenye jukwaa lolote la kisiasa kama ilivyo kwa wasanii wengine, na kumsapoti mgombea
Hisia ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha planet Bongo kinachorushwa na east Africa Radio.

"Niko busy mzee, kuna project nyingi tunafanya kama unafahamu mwaka huu mwezi wa tano kulikuwa kuna shindano la ubalozi wa Ufaranca Burundi, basicaly lilikuwa ni shindano la kutafuta nyimbo amabyo inaweza kusaidia kupromote lugha ya Kifaransa Afrika Mshariki, tulienda tukashiriki na Tanzania ikashinda, mimi ndo nilishinda", alisema Hisia.

Pamoja na hayo Msanii Hisia pia amesema swala la shule limekuwa sababu nyingine kwa sababu yeye kwa sasa anasoma nchini Nairobi.