Sunday , 18th Oct , 2015

Tukiwa tunaelekea kwenye kilele za kampeni za uchaguzi mkuu wa urais, udiwani na ubunge mnamo tarehe 25 mwezi huu October, tayari filamu mpya iliyobatizwa jina 'Maisha ni siasa' inatarajiwa kuzinduliwa rasmi wiki hii jijini Dar es Salaam.

Filamu mpya ya 'Maisha ni Siasa' inayotarajiwa kuwagusa watanzania katika uzinduzi wake hivi karibuni

Filamu hiyo ambayo inazungumzia umuhimu wa mchakato wa kiasiasa ambapo kila mmoja anaathirika kwa namna moja au nyingine kisiasa imeshirikisha wasanii nyota na wengine chipukizi ambao hawajawahi kuigiza Bahati Chando, Godwin Gondwe, Haton Kamwoga na wengine wengi.

Enewz imeongea na Mtayarishaji mahiri wa filamu nchini Tanzania Paul Mashauri ambaye amekuwa na haya ya kusema kuhusiana na filamu hii ambayo inatarajia kuwafikishia ujumbe kwa Watanzania kuelekea katika uchaguzi mkuu wiki
hii.