Friday , 4th Apr , 2014

Kundi bora la muziki Afrika, Mafikizolo limetua leo kwa kishindo Jijini Dar es Salaam tayari kabisa kwa ajili ya kazi moja tu ya kuwarusha mashabiki wa muziki katika bonge la shoo ambayo itafanyika kesho katika ukumbi wa Mlimani City.

Mafikizolo wakiwasili Airport Dar leo

Baada tu ya kutua kwa ndege katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere majira ya mchana eNewz ilihojiana na kundi zima la Mafikizolo, ambapo wamesema wamejipanga katika kutoa burudani kali hapo kesho litakalowaacha Watanzania na kumbukumbu isiyosahaulika.

Kazi inabaki moja tu, ni kwa wewe kudondoka pale Mlimani City siku ya kesho kuanzia majira ya saa moja usiku kwa ajili ya shoo kali ya Mafikizolo inayoletwa kwako na Juegga Cassa kwa udhamini wa nguvu wa East Africa Radio na East Africa Television.