Friday , 31st Jul , 2015

Msanii wa muziki Shilole amefungiwa kujihusisha na sanaa katika kipindi cha mwaka mmoja ili kujirekebisha kimaadili kwa kutumbuiza jukwaani akiwa amevaa nusu utupu katika onyesho lake alilofanya nchini Ubelgiji mwezi Mei mwaka huu.

staa wa miondoko ya bongofleva Zuena Mohammed aka Shilole

Akiitolea ufafanuzi hatua hii, Katibu wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Mngereza amesema, baraza limeamua kuchukua hatua hiyo kufuatia ahadi ya serikali katika Bunge la Bajeti Mei 28 ambapo Mhe. Juma Nkamia alieleza kuwa taratibu zote zitachukuliwa dhidi ya msanii huyo.

Vilevile eNewz imeongea na Shilole na akaelezea vile alivyoipokea hukumu hii nzito inayofunga njia zake kuu za kujipatia kipato cha kuendesha maisha ya kila siku.