Thursday , 5th Jun , 2014

Rais wa kundi la muziki la Tip Top Connection Madee baada ya kudondosha mjengo wake huko Kimara Jijini Dar es Salaam, mashabiki na wadau mbalimbali wamekuwa na shauku ya kujua mipango yake ya kuoa kutokana na maisha yake ya ukapera.

Madee akitumbuiza stejini

Kutokana na kauli hizo Madee ambaye wasichana wengi wamekuwa wakimfuatilia kupitia mitandao ya kijamii ameamua kuweka wazi kuwa hivi sasa hana haraka na swala la kuoa kwani ni muhimu kujipanga na si tu kuvamia kutafuta sifa kwa watu wanokuzunguka.

Mwanamke mwenye sifa ambazo yeye Madee anazitaka ni kwamba ni lazima kwanza ajitambue kuwa Madee ni mtu wa aina gani pia ni lazima ajiheshimu na hiyo ndio sifa kubwa ya mwanamke anayependezwa kuwa naye.

Aidha, Prezidaa huyo wa Manzese ameelezea furaha yake ikiwa ndio mara yake ya kwanza kutumbuiza Kahama ambapo ataongozana na kikosi cha wasanii watakaotumbuiza katika ziara maarufu ya muziki ya Kili Music Tour itakayofanyika Jumamosi hii ya tarehe 07, katika uwanja wa Halmashauri wa Kahama.