Monday , 21st Dec , 2015

Madee ambaye katika ngazi ya familia anatambulika pia kama Baba Saida akiwa anaonyesha kumudu vizuri jukumu lake kama baba, amesema amesitisha shughuli zote za muziki kwa mwisho wa mwaka huu mpaka Januar kupata muda zaidi wa kukaa na binti yake.

Madee

Madee amesema kuwa, huu unakuwa ni wakati muhimu kwake kama baba baada ya kupata rasmi haki ya malezi ya mwanae huyo yaani custody, baada ya kumaliza matatizo ambayo hakupenda kuyaweka wazi, hii ikiwa ni nafasi adhimu ya kukaa na mwanae mpaka atakaporudi shule mwezi Januari mwakani.

Baba Saida pia akatumia nafasi hii kutoa somo la malezi kwa wazazi wenzake, hususan ma-Single Daddies akigusia umuhimu wa kujenga urafiki na watoto wao, kutokana na mambo kubadilika na utandawazi kukuwa, akitaka mzazi kuwa na urafiki mkubwa na mwanae na kumtengenezea mazingira ya kuwa huru kuuliza mzazi chochote kile ambacho wanakumbana nacho, iwe kibaya ama kizuri kwa lengo la kujifunza.