Saturday , 13th May , 2017

Dogo Janja amefunguka na kusema kama isingekuwa rais wa Manzese Madee Ally kumrudisha chini ya usimamizi wake basi angeshaacha muziki na kurudi ngarenaro, na kwamba anamshukuru kwa kuwa anausapoti muziki wake kwa asilimia 100 kama baba mlezi.

Janjaro amefunguka hivi karibuni na kusema kwamba Madee ameokoa kipaji chake na kama angemtelekeza moja kwa moja asingeweza kusikika tena kwenye muziki 

"Madee amenitoa mbali, anamchango wa asilimia 100 kwenye muziki wangu. Nisingerudi tena kwenye 'game'kama asingenirudisha kwake. Nilikuwa kwenye uongozi mwingine kabla sijarudi 'Tip Top connection' lakini nilitoa wimbo mmoja tuu na baada ya hapo nilikaa kimya kwa muda wa miaka mitatu mpaka niliporudi tena kwenye mikono ya Madee nikatoa wimbo mkali ulionirudisha kwenye chati. Madee ni baba mwenye uchungu na mwanaye kwa sababu anajua aliponitoa, kama siyo yeye ningekuwa ngarenaro nakula ugoro- Janjaro.

Akizungumzia kuhusu muziki wake amedai hapendi kufanya kolabo zisizokuwa na mafanikio ndio maana mpaka sasa hana nyimbo zinazozidi tatu alizoshirikshwa na wasanii wenzake.

Kwa sasa Janjaro anatamba na ngoma inayokwenda kwa jina la ukivaaje utapendeza.