Thursday , 5th Feb , 2015

Madee amesema kuwa, anajiamini kwa kila kitu ambacho anakuwa anakifanya sasa kutokana na kuwa na timu kubwa nyuma yake ambayo inahakikisha kuwa yeye pamoja na kile ambacho anakitoa kwa ajili ya mashabiki zake kinaenda sawa.

Msanii kutoka kundi la Tip Top Connection nchini Tanzania Madee

Madee ameiambia eNewz maneno haya ikiwa pia ni utetezi wake kutokana na teaser ya video ya ngoma yake ya 'Vuvula' ambayo imezua gumzo kubwa mtandaoni baada ya watu kuiona na kuhisi kuwa kwa namna moja ama nyingine inakiuka misingi fulani ya kimaadili ya kitanzania.