Maua Sama ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa kwa sasa wasanii wa kike Tanzania wako wachache, na changamoto zilizopo zisiwaogopeshe.
“Muziki una hela kama kuna binti ana kipaji au anaweza kukaa kwenye game tujitahidi, wasichana tuko wachache Tanzania, changamoto zisikufanye ubweteke”, alisema Maua.
Pia Maua amesema wanawake wanayo nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye sanaa, kutokana na mvuto walionao, lakini isiwe sababu ya kujisahau wanapokuwa jukwaani na kukiuka maadili.
Pamoja na hayo Maua ameelezea mipango yake ya sasa baada ya kumaliza shule, na kusema kuwa ana mpango wa kutoa albam yake ya kwanza, ambayo iko ukingoni kuitengeneza.
“Mimi na team tumejipanga, natarajia kufanya video ya mahaba niue, sasa hivi najipanga kwenye albam, naandaa albam ya kwanza na niko mbioni kuimalizia”, alisema Maua.