Monday , 24th Feb , 2014

Staa wa filamu wa kimataifa mwenye asili ya Kenya Lupita Nyong'o, ametolea ufafanuzi tetesi za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwigizaji Jarred Leto ambapo kulingana na majibu yake, hakuna chochote kinachoendelea kati yao.

Akijibu kwa utani swali hili, Lupita amesema kuwa Miley Cyrus ndiye aliyewatenganisha yeye na Leto, na majibu haya ni kutokana na uvumi ambao unaendelea kwa upande mwingine mtaani kuwa Mwigizaji huyu wa kiume ana mahusiano na Miley pia.

Kwa sasa Lupita amekuwa akimulikwa na vyombo mbali mbali vya habari ili kufahamu kwa undani zaidi maisha yake binafsi baada ya kujipatia umaarufu na mafanikio makubwa kutoka kwa filamu ya 12 Years A Slave ambayo ameshiriki kwa umahiri mkubwa ndani yake.