Monday , 21st Sep , 2015

Nyota wa filamu wa kimataifa Lupita Nyong'o amekwapua nafasi nyingine kubwa ya kushiriki katika toleo jipya la filamu maarufu ya zamani ya 'Jungle Book inayotayarishwa na Disney ya wahusika wa kutengeneza.

Nyota wa filamu wa kimataifa Lupita Nyong'o wa nchini Kenya

Ndani ya uhusika wake katika filamu huyo Lupita atavaa uhusika akitambulika kama Raksha ambayo taarifa zaidi ni kwamba filamu itaingia rasmi sokoni mwezi Aprili mwaka 2016, itahusisha pia mastaa wengine wakubwa kutoka Hollywood akiwepo Idris Alba, Scarlett Johansson , Christopher Walken na Neel Sethi.

Filamu ya kwanza kabisa ya Jungle Book ilitoka mwaka 1967, waratibu wakiona kila sababu ya kufanya tena projekti hiyo kwa kutumia bajeti ya kutosha, na kwenda sawia na mabadiliko makubwa ya ki-teknolojia katika kutayarisha filamu za wahusika wa kutengeneza - yaani Animation.