
Muongozaji wa video za kibongo Msafiri Shabani
Akizungumza na Enewz Msafiri alisema kuwa ni kutokana na uhakika na uharaka wa upatikanaji wa vitu kwaajili ya kazi zao kwakuwa kwa Tanzania inachukua muda mrefu wa kupata ruhusa ya kukamirisha kazi zao.
“unakuta unaambiwa uandike barua, barua yenyewe inaweza ikaenda kujadiliwa mpaka wewe unakuja kupewe jibu tayari umeshaenda South Afrika umesghuti na tayari video umeshatoa hata katika lokesheni unakuta mtu mpaka akugeie gari ama nyumba mpaka muwe munajuana akati ukienda South chochote unachokitaka vipo vya kukodi ni wewe tu ukiwa na pesa”,alisema Msafiri
Pia Msafiri aliongezea kuwa sababu nyingine inayowafanya wakashuti video hizo nnje ni kutokana na kuangalia wengine wanafanya nini ili nao waweze kushika nafasi nzuri katika soko la ushindani pia akidai kuwa inasaidia kupandisha value ya msanii kwakuwa anaonekana anauwezo wa kutengeneza pesa kwaajili ya kufanya kazi zake.