Wednesday , 1st Feb , 2017

Msanii wa bongo fleva Linex ameelezea maana ya wimbo wake alioupa jina la 'Kiherehere' na kuwashauri watu wanaojiingiza katika mapenzi kuacha kiherehere.

Linex

 

Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Linex amesema maana halisi ya kiherehere ni kimuhemuhe cha kufanya jambo ambalo baadaye linaweza likakuumiza katika maisha yako lakini bado unataka kufanya kwani watu wengi hujua kwamba mapenzi yanaumiza lakini bado hawakomi wanaendelea kuwapenda watu.

Linex hakusita kusema kwamba kwa sasa amepunguza kula bata na kuhifadhi fedha yake kwa ajili ya familia yake na maisha yake ya  baadaye kwa ajili ya watoto wake.