Saturday , 24th Jan , 2015

Katika kuhakikisha kuwa anaendelea kufanya kazi katika ubora na viwango vya Kimataifa, msanii wa muziki Linah Sanga a.k.a Ndege Mnana ametambulisha ujio mpya.

Linah Sanga a.k.a Ndege Mnana

Ujio huo ni wa kazi yake mpya inayokwenda kwa jina No Stress, ikiwa na mikono ya watayarishaji kutoka ndani na nje ya nchi.

Linah ambaye leo atakuwa live akimwaga burudani katika jukwaa la Tigo Kiboko Yao amesema kuwa, kwa sasa anajitahidi sana rekodi zake zote ziwe zina-sound katika kiwango kile kile cha Ole Themba, na hivyo ngoma yake mpya itakuwa ni miguso ya Nash Designer, huku mixing ikifanywa na mtayarishaji wa kimataifa anayetambulika kwa jina Busi.