Flora Mbasha
Frorah Mbasha amesema kuwa, anamshukuru Mungu kwa kufanikisha kutoa albam mpya inayokwenda kwa jina Nipe Nguvu ya Kushinda, kazi ambayo tayari jamii imeipokea vizuri.
Msanii huyu ambaye amezoeleka kufanya kazi ya muziki pamoja na mumewe Emmanuel Mbasha, amewatoa wasiwasi mashabiki kuwa licha ya mgogoro, Mumewe yupo katika kazi hii.