Matonya
Tonya-business amesema kusajiliwa katika vikundi hivyo ni kupoteza muda ila endapo wasanii wenzake watahitaji kuweka akili zao pamoja ili waweze kutengeneza jambo litakalokuwa na faida kwa kila mmoja yupo tayari kwa hilo.
“Mimi sasa hivi siko tayari kwenda kufanya kazi sijui kusajiliwa ‘label’ siko tayari, labda kuweka akili zetu sehemu moja kuhakikisha kila kitu tunakiweka sawa niko tayari kwa sababu sisi sote tunapigania njia moja ni kuweka nguvu kwa ajili ya kusogeza muziki wetu”. Alisema Matonya
Hata hivyo siyo mara ya kwanza kutokea kwa kauli kama hizo kwa maana hata juzi kati msanii Mrisho Mpoto alitoa wazo la wasanii kukutana na kufanya jambo kwa pamoja ili waweze kuitwa wasanii wa Taifa la Tanzania na siyo msanii wa kutoka katika ‘lebo’ fulani.

