Kim Kardashian ambaye ni dada wa Khloe amepost picha inawaonyesha wanatembea wakiwa na Lamar, ambayo inadhihirisha wazi kuimarika kwake, kitendo ambacho watu wengi hawakutarajia kutokana na hali ngumu aliyokuwa nayo kipindi cha nyuma
kwenye picha hiyo Kim Kardashian aliandika maneno haya.. “Super Soul Sunday time before Super Bowl Sunday time with Khloe and Lamar”.
Lamar Odom alipata matatizo a ubongo baada ya kupoteza fahamu kulikosababishwa na matumizi makubwa ya madawa, ambako pia alipoteza kumbukumbu na kushindwa kutambua hata familia yake, pamoja na kushindwa kutembea.
Hivi Karibuni Lamar Odom alitolewa hospitali alipokuwa akitibiwa, na kupelekwa kwenye kituo kingine cha matibabu ya kimwili. (physiotherapy), na taarifa zinasema kwa sasa ameweza kurudisha kumbukumbu, na hata kuweza kuongea.








