Mavoko amyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba nayo ni moja ya kujivunia kile anachokifanya.
"Mtu mwengine inawezekana anapost vitu au nyumba, au gari au pesa, kwa kutoa shukrani kwa watu ambao wamemfanya mpaka awe hapo, ina maana ni hao watu ndio anaowapostia, ili waone kwamba sasa hivi nimepiga hatua kiasi gani", alisema Mavoko kwenye mazungumzo yake na timu ya Planet Bongo.
Mavoko pia alisema kwa upande wa pili kitendo hicho sio kizuri, kwani kinaonyesha majivuno ambayo si kutu kizuri kwa jamii.
"Kuna mtu anaonyesha hivyo vitu kwa kujivuna kwamba nimepata na nini, hakuna mtu mwenye pesa zaidi yangu, au mi niko na pesa sasa hivi, kwa hiyo ni mbaya", alisema Mavoko.