Friday , 20th Jun , 2014

Msanii wa muziki Habib Koite kutoka nchini Mali atashiriki leo hii katika onyesha la muziki Jijini Dar es Salaam kuadhimisha siku ya muziki duniani.

Msanii wa nchini Mali Habib Koite akicharaza gitaa

Msanii huyo amesema kuwa, muziki umebakia kuwa njia ya pekee yenye nguvu ya kuwaleta watu wa hulka, dini, imani na tamaduni tofauti pamoja.

Habib katika mahojiano maalum aliyofanya na eNewz, amesema kuwa muziki kwa namna ya pekee umeweza kuunganisha watu na kuburudika pamoja licha ya tofauti kubwa za asili, na tafsiri zao katika mambo mbalimbali, kama anavyoeleza mwenyewe hapa.

Koite ameongezea kuwa kuna hazina kubwa ya muziki iliyopo ndani ya bara la Afrika kwani bara hili lina vipaji vingi ambavyo ni dalili nzuri ya kuufikisha muziki wake mbali.