Wednesday , 23rd Apr , 2014

Msanii wa muziki Koffi Olomide kutoka nchini Congo, anatarajiwa kutua nchini Uganda na kufanya onesho Ijumaa hii tarehe 25, katika tukio kubwa lililoandaliwa na klabu ya Rotary nchini humo kwa lengo la kuhamasisha watu juu ya uchangiaji wa damu.

Koffi Olomide, anatarajiwa kufanya kazi ya ziada kutumbuiza washiriki wa tukio hili kubwa la kijamii, akiwa na sapoti kubwa ya bendi yake mahiri ya muziki, huku muziki wake ukiwa na rekodi ya kufanya vizuri zaidi huko Uganda katika miaka ya 90.

Onesho hili la msanii huyu mkubwa Afrika, linatarajia kuwa ni la mafanikio makubwa licha ya mapambano dhidi ya muziki wa kigeni yanayoendelea sasa nchini humo kati ya wadau wa muziki wasanii na vyombo vya habari.