
Hivi karibuni Msaga Sumu alizungumza na eNewz na kubainisha kuwa wasanii wengi wa singeli hawana ubunifu, na ndiyo sababu muziki huo unaelekea kuwa kwa kuwa wanashindwa kutoa kazi zenye utofauti, huku akijiita kuwa yeye ndiye mfalme wa singeli Tanzania.
Akionge kupitia kipindi cha eNewz cha EATV, Man Fongo amesema "Kama anasema kwamba sisi hatuna uwezo siyo kweli na kama kweli yeye ni mfalme mbona hajaachia nyimbo tangu mwaka huu uanze? Mimi nitaachia nyimbo tuone kama haita sikika. Namuona Msaga Sumu kwangu bado kabisa kwa kuwa tunaimba aina tofauti ya muziki"
Hii ni ishara kuwa huenda Man Fongo akawa anakerwa zaidi na Msaga Sumu kujiita Mfalme wa Singeli
Hata hivyo Man Fongo amewasihi wasanii wa nyimbo za singeli kupendana ili kuweza kufanya mapinduzi makubwa katika muziki na kuweza kwenda sawa na muziki wa bongo fleva