Tuesday , 14th Apr , 2015

Staa wa muziki Eddy Kenzo kutoka nchini Uganda, ameshiriki katika mbio za Kabaka sambamba na kulipia zaidi ya watu 30 ada ya kushiriki mbio hizo kuchangisha fedha za kupambana na ugonjwa wa Fistula.

msanii wa muziki nchini Uganda Eddy Kenzo

Msanii huyu ameshiriki katika zoezi hilo sambamba na umati mkubwa wa washiriki kutoka jamii ya Baganda, hii ikiwa ni sehemu ya kurejesha fadhila kwa jamii kutokana na mafanikio yake kimuziki.

Eddy Kenzo ambaye amejijengea jina kubwa kupitia ngoma yake ya Sitya Loss,ambaye hivi sasa anatamba na remix ya ngoma yake ya Jambolee akiwa ameshirikisha msanii Kcee kutoka Nigeria.