Monday , 24th Mar , 2014

Msanii Kenzo kutoka nchini Kenya, baada ya kutangaza kuwa mambo yake sasa yameanza kumnyookea baada ya kutoka chini ya usimamizi ya lebo ya Ogopa, ameweka wazi kuwa kwa sasa yupo katika hatua za mwisho za makubaliano kuingia katika mkataba huo.

Kenzo amesema kuwa, katika mkataba huu mpya atakaoingia, atakuwa na uhuru wa kurekodi kazi zake sehemu nyingine yoyote ile, tofauti na mkataba wa awali ambao ulikuwa ukimbana kufanya kazi sehemu moja.

Endapo mipango hii ya Kenzo itanyooka kama matarajio yake yalivyo, itakuwa ni nafasi nyingine kubwa ya msanii huyu kuweza kufanikiwa kuingia kwa nguvu katika soko la muziki la Kimataifa.

Tags: