Thursday , 5th Feb , 2015

Msanii mkongwe katika gemu ya Hip hop hapa Bongo, Kalapina amesema kuwa ngoma yake mpya ya Good Time ambayo amemshirikisha Ommy Dimpoz ndani yake, imekuwa ni kazi ambayo imemletea mafanikio makubwa na kumuongezea mashabiki zaidi hasa wale wa kike.

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Kalapina na Ommy Dimpoz

Kalapina amesema kuwa, kwa muda mrefu hakuwa amehusisha ishu ya mapenzi katika kazi zake, na baada ya kuamua kufanya kazi ya aina hiyo na kumshirikisha mwana bongo flava Ommy Dimpoz, anaweza kusema kuwa rekodi hii imekuwa ni ngoma ya hip hop inayochezwa na pia kununuliwa mtandaoni zaidi.