Friday , 7th Aug , 2015

Katika muendelezo wa upepo wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba, msanii na mwanaharakati Kala Jeremiah, ametoa angalizo kwa watanzania kutokufuata kundi la watu kufanya uchaguzi wao, bali wasimame kupima uwezo wa viongozi husika.

staa wa muziki wa miondoko ya bongofleva Kala Jeremiah

Kala ambaye ni moja ya marapa ambao msimamo wao kisiasa umezingwa na msimamo wake huo, amesema kuwa ni suala la busara kwa Watanzania, kuangalia mtu mmoja mmoja kutoka kila chama kutokana na uwezo wa viongozi na misimamo yao kutofautiana.