Kuhusiana na kazi hii mpya Kala Pina ameongea na mashabiki wake kupitia eNewz ambapo amesema kuwa huu ni ujio tofauti kabisa kutoka kwake na maalum kwa ajili ya kuleta mapinduzi katika muziki wa Bongo ambao amesema kwa sasa umeshikilia muziki wa aina fulani tu.
Kala pina amesema kuwa, kazi hii mpya itatoka mapema wiki ijayo na ameeleza kuwa atatoa nafasi kwa mashabiki kuisikiliza kwa mara ya kwanza kupitia East Africa Radio.