
Akiongea kupitia eNEWZ ya East Africa Television Kala amesema "nimefanya mziki kwa mda mrefu ila sijawahi kupata pongezi kutoka kwa kiongozi mkubwa wa nchi kama yule tena mbele za maelfu ya watu mara nyingi tumekuwa tukikutana na viongozi wa kawaida na kutupa pongezi za kawaida”.
Kala ameongeza kuwa alizipokea salamu za Makamu wa Rais kutoka kwa watu wengi kitendo ambacho amekipokea kwa mikono miwili na kuwa kauli hiyo ya Makamu wa Rais imempa deni la kuendelea kukaza buti na kuandaa nyimbo nyingi zitakazo kuwa mkombozi kwa Jamii.
Kala amemaliza kwa kusema kauli ya Makamu wa Rais imempa faraja yeye na familia yake kwa ujumla na hata alipotumiwa kile kipande cha video ambayo Makam wa Rais alikuwa anamsifia aliiangalia mara nyingi kiasi kwamba hakuamini kitu ambacho alikuwa anakiona.
Msanii huyo wa Hip Hop kutoka Rock City anafunga mwaka kwa kauli yake ya kuwa hakuna mziki wa biashara bali kuna biashara ya muziki aliyoitoa hivi karibuni kupitia Enewz.