Wednesday , 8th Jul , 2015

Aliyewahi kuwa mshiriki wa shindano maarufu la kipindi cha maisha ya uhalisia nchini Afrika Kusini Julio Batalia wa nchini Tanzania kwa mara ya kwanza amesema ataanza kuonesha uwezo wake katika sanaa kwa kuanza kuimba solo.

msanii wa miondoko ya bongofleva Julio Batalia

Julio anataka kuwaonesha mashabiki wake kuwa uwezo wa kusimama yeye mwenyewe kama msanii wa kujitegemea anao na si kwamba kolabo pekee ndizo zinazomfanya ainuke kisanaa, huku pia akijipanga kuingia studio kutoa kibao chake kipya ambacho hakika kitamweka katika ngazi za kimataifa zaidi.