Saturday , 19th Apr , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Kenya, Juliani baada ya kufanya vizuri sana katika soko la muziki na Albam zake mbili za kwanza, kwa sasa msanii huyu anatarajia kuachia albam yake ya tatu, ambayo tayari imekwishakamilika sasa.

Juliani

Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia, Albam hii mpya ya Juliani inatarajiwa kuwasilishwa kwa wadau wakubwa wa muziki Kenya kwa ajili ya kuisikiliza, katika sherehe maalum inayofahamika kama 'Listening Party' ambayo itafanyika wiki ijayo jijini Nairobi.

Albam hii itabeba kazi kali kabisa za msanii huyu, ikiwepo rekodi ya Utawala ambayo iliweza kufanya vizuri zaidi mwaka jana ndani na nje ya Afrika Mashariki.

Tags: