Monday , 16th Mar , 2015

Rapa Jua Cali kutoka nchini Kenya, akiwa kama balozi wa mbio za riadha za Lari zenye lengo la kuchanga fedha za kuhifadhi msitu mkubwa wa Kereita, anatarajia kuwa sehemu ya upandaji wa miti zaidi ya 50,000, zoezi litakaloenda sambamba na mbio hizo.

msanii wa muziki wa nchini Kenya Jua Cali

Mbio hizo ambazo zitafanyika Jumamosi tarehe 28 mwezi huu, pia kupitia washiriki wake zinatarajiwa kuchanga fedha ambazo zitatumika kuendeleza na kuhifadhi uhalisia na vivutio vya utalii ambao unapatikana ndani ya msitu huo.

Kushirikishwa kwa Jua Cali katika mpango huo ni katika jitihada za kufikia kundi kubwa zaidi la watu hususan vijana, kufahamu na vilevile kushiriki katika tukio hili lenye umuhimu mkubwa kwa mustakabali wa mazingira.