Sunday , 13th Dec , 2015

Neno 'Mama' linaendelea kupewa heshima kila kona ya dunia kupitia nyimbo ambazo zinawasifu kutokana na malezi yao ambapo msanii wa bongofleva John Rodgers ameamua kurudisha shukrani zake za dhati kwa mama yake mzazi kupitia video ya wimbo wake mpya.

msanii wa miondoko ya bongofleva John Rodgers

Msanii huyo aliyeubatiza wimbo huo mpya kwa jina la 'Mama' ambaye aliyeibuka vyema katika game baada ya kufanya ngoma na msanii shillah iitwayo 'You Make my Heart Sing' amesema hii ni project yake mpya ambayo ni mahususi kwa ajili ya shukrani na malezi mema kutoka kwa mama yake.