Monday , 9th Jun , 2014

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete leo amewaongoza mamia ya wakazi wa jiji la DSM katika maziko ya msanii nguli wa maigizo Said Ngamba au Mzee Small.

Rais Kikwete akiongoza dua ya kumuombea Marehemu Mzee Small muda mfupi kabla ya maziko yake

Aliyekuwa mwigizaji maarufu wa filamu nchini, Marehemu Mzee Small amezikwa leo jijini Dar es Salaam katika makaburi ya Tabata Segerea akisindikizwa katika safari yake ya mwisho na umati mkubwa wa waombolezaji, wasanii na wadau mbalimbali, wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete aliyeongozana na mkewe mama Salma Kikwete.

Mzee Small ambaye atakumbukwa kwa umahiri wake katika sanaa ya filamu hususan akiwa na mwigizaji mwenzake Bi. Chau, alizaliwa miaka 59 iliyopita, amefikwa na umauti baada ya kuugua ugonjwa wa kiharusi tangu mwaka 2012.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.Amen.