
Aika (kushoto), Vanessa (Kulia)
Msanii huyo alibainisha hayo jana wakati akizungumza katika kipindi cha Ngaz kwa Ngaz cha EATV kinachorushwa kila Alhamisi kuanzia saa tatu kamili usiku na kusema kuwa anamshukuru sana Vee Money kwa kumrudisha katika mzunguko wa muziki baada ya yeye kukata tamaa pindi alipoingia katika soko hilo.
“Vee Money ni msichana mwenye bidii pia ametu’motivate vitu vingi kwenye maisha yetu, maana ilifikia wakati tulikata tamaa kuendelea na muziki”. Alisema Aika
Aidha msanii huyo aliendelea kufunguka na kusema pindi VeeMoney alipo watembelea katika studioni zao na kusikiliza vionjo vya wimbo wao chelewa aliwaamuru waiachie ngoma hiyo kwa jamii kwakuwa imebeba ‘melody’ nzuri
“Yeye ndiye alitufanya sisi turudi kwenye muziki baada ya kuja studio na kusikiliza nyimbo zetu na kusema ‘jamani toeni huu wimbo wa Chelewa ‘by then’,amekuwa akitu‘encourage’ na tukisaidiana sana”. Alifafanua zaidi Aika