msanii wa nchini Kenya Jimmy Gait
Kazi hii mpya inakwenda kwa jina 'Mzuka Huu', na imeweza kwa kiasi kikubwa kurudisha mioyo ya mashabiki wengi, hususan wale ambao walikuwa na mtazamo kuwa msanii huyu anatoka nje ya misingi ya muziki wa injili kupitia kazi yake ya 'Makeke'.
Mapokezi mazuri ya kazi hii mpya ya Jimmy Gait, ni ishara ya mafanikio na vilevile moyo wa shukrani alio nao, hususan kwa wale wote ambao amekuwa akishirikiana nao katika kazi zake kila siku.