Monday , 12th Jun , 2017

Mkongwe aliyerudi kwenye game kwa kasi nzuri, Juma Mchopanga 'Jay Moe' amefunguka na kusema kwamba kwenye nyimbo zake alizoweza kuandika na ku-diss watumiaji wa unga ilikuwa ni njia ya kufikisha ujumbe kwa marafiki zake na wasanii kwa njia ya sanaa.

Mwanamuziki Juma Mchopanga 'Jay Moe'

Jay Moe ameweka wazi hayo baada ya kuulizwa juu ya mstari wake ' bora mimi sikuwa na zali maana waliopata zali sasa hivi ni mateja hatari" kuwa ni kweli aliandika kwa ajili kuwadiss wasanii wenzake waliokuwa wanatumia madawa ya kulevya.

Jay Moe amesema kuwa kwa muda mwingi amekuwa balozi wa kukemea matumizi ya dawa za kulevya kwa wasanii kwani imekuwa ikileta picha mbaya kwa wazazi ambao wataanza kuwaza kama mwanaye akiwa msanii basi baadae akipata umaarufu lazima atajidumbukiza hwenye dawa za kulevya.

"Mimi nmezaliwa katika mazingira ya dini na yanayofundisha kutokukata  tamaa. Sasa wasanii wanaotumia vigezo vya game ngumu ndio maana wanaingia kwenye madawa ni uongo, kwa sababu kutumia madawa ni kukata tamaa ya kuhangaika kama kijana . Lakini kama unaweza ukaaingia kwenye madawa ukawa unatumia hata laki kwa kusema unamaliza stress ugumu wa game unakuja vipi hapo. Tatizo wengi wao wanashindwa ku-confess kama kuiga iga ndo kumewaponza. Mwisho wa siku wanakuja kutuchoresha sisi wengine ambao tunapambana kuwaaminisha wazazi huu muziki siyo uhuni.

Mwanamuziki Jay Moe

"Aidha Jay ameongeza kuwa "Nilitumia wimbo kuwachana hadi washkaji zangu kwa sababu najua ingewatia hasira kuliko ningemwambia tukiwa wawili, ningemuambia kishkaji lakini kwenye ngoma inasikilizwa na mamilioni ya watu hivyo mtu anajishtukia na wapo watu wengi walikuja ku confess wameacha na wengine wamehitaji ushauri. Jay Moe aliongeza.