Thursday , 30th Apr , 2015

Staa wa muziki Izzo Business, amegusia suala la maadili katika mitindo ya mavazi hususan kwa wasanii na kueleza kuwa, kwa mpango wa Mungu kila sekta imekuwa na mtindo na muonekano ambao humsaidia mtu kutambua muhusika kwa mara ya kwanza.

msanii wa bongofleva Izzo Bizness

Izzo ambaye ametoa angalizo kuwa hatetei mitindo mibaya ambayo inaigwa ikiwemo kushusha suruali - mlegezo, akitetea uvaaji wa wasanii kwa sasa, amesema umetokana na watu ambao wamewavuta kuingia katika muziki.